DKT MPANGO AINYOOSHEA KIDOLE UWT PWANI

 Na Shushu Joel, Kibaha 

Makamu wa Rais Dkt Philip Isdor Mpango akisisitiza jambo kwa viongozi mbalimbali wa CCM (NA SHUSHU JOEL)

MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani  ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Isdor Mpango ameionya Jumuiya ya Wanawake Tanzania ( UWT) Mkoa wa Pwani juu ya uwepo wa makundi ya kutokupendana na kupelekea kuwepo kwa chuki na hata kutokufanyika kwa shughuli nyingi za jumuiya hiyo Hivyo amemtaka Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kuhakikisha kuvunja mara moja makurdi wanayoyaendeleza ndani ya jumuiya hiyo.


Akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa mikutano wa Mwl Nyerere Makamu wa Rais Philip Isdor Mpango  Dkt Philip Isdor Mpango alisema kuwa UWT bado kuna changamoto nyingi za uwepo wa makurdi kitu ambacho ni kibaya sana kwa Karne  ya sasa.


Aidha Makamu  huyo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Mpango alisema kuwa Chama kinatambua kuwa Wanawake ni jeshi kubwa lakini pasipo  na uwepo wa makurdi ya kisiasa ya kusema kuwa mimi ni wa huyu na mwingine ni yule.

Wajumbe wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt nMpango

"Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani nenda kamalize makurdi kwani ni hatari sana kwa maendeleo ya chama chetu cha CCM" Alisema Mlezi huyo wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.


Pia amewakumbusha viongozi wa Chama kutembea kifua mbele kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi na hasa kwenye Mkoa huu wa Pwani , Hivyo niwatake muweze kuwaeleza wananchi kile kilichofanywa na Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan

MWISHO

Post a Comment

0 Comments