MWENYEKITI UWT KIBAHA VIJIJINI ASHUSHA NEEMA KWA WANAFUNZI.

 Na Shushu Joel, Kibaha

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kibaha akiwa na faini ya kolaba(SHUSHU JOEL





SENYEKITI  wa Jumiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya kibaha vijijini Bi Leila Hamoud Jumaa ameshusha neema kwa wananfunzi wa shule ya Msingi Gumba iliyoko katika kata ya Gwata.


Akizungumza mara baada ya zoezi hilo la ugawaji wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa wavulana na wasichana Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo ni kuhamasisha michezo mashule ili kuisaidia serikali katika sekta ya michezo. 


"Kama Mwenyekiti wa Wanawake wilaya ya Kibaha vijijini natambua thamani ya kukuza vipaji vya watoto na ni lazima vianzie chini ili kusaidia Taifa hili kuendelea kuwa na vijana wenye vipaji" Alisema Mwenyekiti huyo Bi, Leila.


Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa jumuiya hiyo itaendelea kutoa sapoti  kwa vijana walioko mashule ni kwa kusaidia vifaa mbalimbali vya kimichezo kwa kusudi la kuwaunga mkono na kukuza vipaji vyao ambavyo vitakuja kuwa msaada mkubwa kwa Taifa letu.


Pia amewataka kuvitumia vifaa hivyo kwa uzuri ili vidumu kwa muda mrefu .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments