Na Shushu Joel, Bagamoyo
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Abubakari Mlawa amewataka wana chama wote kuonyesha malezi yaliyo imara kwa vijana wetu ili kuendeleza kizazi chenye baraka na nuru kwa Taifa letu.
![]() |
Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Bagamoyo akiwa katika moja ya majukumu ya kuzungumza na wazazi(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa HABARI MPYA MEDIA mara baada mahojiano maalum juu ya kuporomoka kwa maadili kwa watoto.
Mlawa alisema kuwa Wazazi sote tunapaswa kuungana ili kusaidia Vijana wetu ili waweze kuwa na maadili mema kama tuliyoyapata sisi enzi za ujana wetu kutoka kwa Wazazi wetu.
" Miaka sie tunazaliwa ukifanya kosa unaonywa na mzazi yeyote yule na ukienda nyumbani unalia basi na kwenyewe unaongezewa hadhabu kitu ambacho klwa sasa hakipo tena" Alisema Mlawa.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Wazazi wilaya hiyo ya Bagamoyo amewakumbusha wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao kila hatua wanazipiga ili kujua nini wanakifanya na kwa wakati gani.
Aidha amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbusha wazazi kuendelea kutambua wajibu wao kwa malezi yenye tija kwa watoto.
Naye Hidaya Nudini ni mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo amempongeza Mwenyekiti huyo kwa nasaha zake kwa lengo la kuwa na Taifa lenye nidhamu.
Aidha amemuomba Mwenyekiti Mlawa kufanya vikao na jumuiya hiyo kwa kila kata kwa lengo la kutoa maelekezo juu ya Mwelekeo wa Taifa letu kwa vijana wetu wa kesho.
MWISHO
0 Comments