MGALU AWATAKA WANAWAKE KUENDELEA KUCHANGAMKIA FURSA.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo 

Subira Mgalu Mbunge wa viti maalum Pwani akiangalia moja ya ubunifu wa nguo uliofanywa na baadhi ya vikundi vya wanawake ( NA SHUSHU JOEL)

MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Subira Mgalu amewakumbusha wanawake wote kuendelea kuchangamkia fursa za upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka halmashauri  mbalimbali hapa nchini kwa kusudi la kukuza uchumi wao .


Akizungumza  katika mafunzo ya ujasiliamali ya kidigital yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge vilivyoko katika wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, Mbunge Mhe Mgalu alisema kuwa Wanawake wamekuwa mstali wa mbele sana katika ukuzaji wa uchumi kupitia nyanga mbalimbali za kibiashara.


Aidha aliongeza kuwa Wanawake ni nguzo kubwa katika ukuzaji wa uchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa hivyo tuendelee kujituma ili kujiongezea kipata zaidi ya hapo tulipo sasa.


" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo kikubwa sana kwa wanawake katika masuala ya ukuzaji wa uchumi kwa kina Mama ndio maana wakati akiwa makamu wa Rais alianzisha majukwaa ya ukuzaji uchumi kwa Wanawake na sasa anazidi kuyasimamia ili yaweze kuwawezesha wanawake zaidi" Alisema Mgalu.


Aidha Mgalu amewataka wanawake kutumia mafunzo hayo ya kidigital kwa wanawake kama fursa ili kuweza kukuza uchumi wao na kuondokana na umasikini.


Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu ( LHRC) Anna Henga ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa jinsi ambavyo umekuwa  mstali wa mbele katika kuchangamkia fursa na hata kupambana na ukatili wa kijinsia.



Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo Ndugu Mohamed Usinga amewahakikishia Wanawake kuwa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo imefungua milango kwa mikopo ya kina Mama .


Aidha Alisema kuwa kutokana na jinsi wilaya ya Bagamoyo  inavyowasamini  wanawake ndio maana itazidi kuwakopesha ili waweze kukuza kukuza mitaji yao kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments