Na Shushu Joel, Chalinze.
![]() |
Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafaua jambo kwa wananchi jinsi gani miradi inavyozidi kutekelezeka ( NA SHUSHU JOEL) |
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa na maono makubwa ya maendeleo kwa watanzania ambao walikuwa na kiu kubwa ya kuyaona.
Akizungumza na Wananchi wa kata ya Pera Naibu Waziri Kikwete alisema kuwa Rais Dkt Samia amewaonyesha watanzania dhamira yake kubwa aliyonayo ya kulijenga Taifa hili ndio maana amekuwa amekuwa mtendaji wa aina ya pekee katika utatuzi wa kero na ufanisi maendeleo umezidi kuongezeka.
Aidha Kikwete alisema kuwa mpaka sasa hakuna mradi uliosimama hivyo hii ni ishara kubwa kwa wananchi ikionyesha namna gani Rais wetu anavyopiga kazi za kuwapambania na kuwafanikishia maendeleo wananchi wake.
:Kutokana na jinsi gani ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejitolea kuleta maendeleo ya kutosha kwetu hivyo kikubwa tunatakiwa kuunga mkono juhudi zake anazozifanya kwetu ili kuweza kumpa moyo" Alisema Kikwete.
Mbali na hayo Kikwete amewakumbusha viongozi kuendelea kuyasema yale yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili jamii yetu ijue .
Naye Jackson Mkango Diwani wa kata ya Pera amemsifu Mbunge kwa ushawishi wake kwa serikali na kuweza kuleta maendeleo tunayoyahitaji kwetu.
"Sisi kwa kushirikiana na wananchi tutaendeleza Dua kwa viongozi wetu ili waendelee kupiga kazi na kuleta maendeleo kama ilivyo kwa Mhe. Ridhiwani Kikwete " Alisema Mkango
MWISHO
0 Comments