“UWT TEMBEENI KIFUA MBELE” RC KUNENGE

Na Shushu Joel, Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutembea kifua mbele kutokana na yale yanayofanywa na Rais wa Jmhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Taifa hili.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa UWT Taifa na Mkoa wa Pwani mara baada ya kikao kazi. ( NA SHUSHU JOEL)


Akizungumza kwenye kikao kazi na Mwenyekiti wa UWT Tiafa Bi, Mery Chatanda Rc Kunenge alisema kuwa hiki ni kipindi chenu kutamba kutokana na utendaji wa hali ya juu unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


“Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa pekee katika dunia hii kutokana ushawishi wake mkubwa ambao amekuwa akiufanywa kwenye mataifa mbalimbali” Alisema Kunenge.


Aidha amewapongeza viongozi wa UWT Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano mkubwa wanampatia katika utekelezaji wa majukumu yake.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi, Mery Chatanda amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika chama na hii ndio sahihi katika utendaji shirikishi kati ya chama na serikali tunaouhitaji.


Aidha Bi, Chatanda amemtaka Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa miongoni mwa watekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi kwa usimamizi uliotukuka wa miaradi ya maendeleo kwa jamii.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments