Na Shushu Joel, Kibaha
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi, Mery Chatanda amewataka wanawake katika Mkoa wa Pwani kutokuwa waoga katika kudhubutu kuchukua fomu za kuwa viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali.
![]() |
Mwenyekiti wa UWT Mery Chatanda akisisitiza jambo kwa baadhi ya viongozi wa jumuiya hiyo waliojitokeza kumpokea katika Mkoa WA Pwani ( NA SHUSHU JOE) |
Akizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo Bi Chatanda alisema kuwa Wanawake ni viongozi wenye maono makubwa kwa jamii zinazowazunguka na ndio maana wamekuwa wakifanikisha maendeleo kwa kiwango cha juu kwenye miradi mingi
" Leo hii Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa kielelezo kikubwa kwenye utendaji wa shughuli za maendeleo kitaifa na kimataifa" Alisema Bi, Chatanda
Aidha amewakumbusha kuendelea kumsemea Rais wetu kwa yale anayoyatenda kwa wananchi kwani Mkoa wa Pwani umefanyiwa mambo makubwa katika maendeleo mbalimbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu amempongeza Mwenyekiti huyo kwa ushauri wake wa kuwataka wanawake kuchangamkia fursa za uongozi ili kuweza kuisaidia jumuiya katika shughuli mbalimbali.
Pia amewapongeza viongozi wote wa UWT ngazibza Mkoa na Wilaya kwa ushiriki wao wa mapokezi ya Mwenyekiti Taifa.
Aidha amewataka kuendelea kuwa na moyo huo huo wa kuwalaki viongozi kwa upendo wa dhati na hii ni kawaida yetu wana Pwani.
MWISHO
0 Comments