NA SHUSHU JOEL
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameileza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuanzisha kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za Muungano.
Waziri Jafo akifafanua jambo jinsi ambavyo wanakwenda kituo cha nyaraka za muungano |
Amesema
hayo leo Machi 24, 2023 jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Kupokea na kujadili
Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa
Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa
Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati hiyo.
Dkt.
Jafo amesema Mungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kuimarika kutokana na
upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi na hivyo kuufanya uwe wa kipekee
duniani.
Amesema Serikali itafanya
ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Pamoja na yale
masuala 22 ya Muungano kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika ipasavyo.
“Ofisi
ya Makamu wa Rais kupitia wataalamu wetu itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu
Muungano na faida zake kwa jamii kupitia vyombo vya habari na maadhimisho
mbalimbali. Aidha, ili kuboresha utoaji elimu kwa umma, Ofisi imeandaa Kitabu
cha Historia ya Muungano kitakachotumika kuelimisha umma kuhusu faida za
Muungano kiuchumi, kijamii na kiutamadun“ amesema.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Joseph Mhagama pamoja na
baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa
taarifa nzuri.
Wamesema kuna umuhimu wa
kutoa ufafanuzi kuhusu hoja za Muungano zilizotatuliwa ili wananchi wapate
uelewa kuhusu mambo gani yaliyopata ufumbuzi kwa pande zote mbili za Muungano.
0 Comments