MARIAM ULEGA ASHUSHA NEEMA KWA VIZIWI

Na Shushu Joel

Mariam Ulega akiwakabidhi viongozi wa Shivyawata zawadi (NA SHUSHU JOE)

MWENYEKITI wa Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi kutokea Mkoa wa Pwani Bi, Mariam Ulega amekutana na watu wasiosikia  ( Viziwi) kupitia kwenye taasisi yao ya shivyawata na kufanikiwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji hao.

Akizungumza wakati alipokuwa akiwakabidhi mahitaji hayo Mariam Ulega alisema kuwa ameguswa na watu hao wenye uhitaji na ndio maana amewasaidia vitu hivyo.

Aidha alisema Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatambua uwepo wa watu hao hivyo naye amekuwa kiungo kikubwa  kwa wahitaji kama nyie ndio maana amekuwa akitoa misaada mingi kwa wahitaji ili waweze kujikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

“Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha ili kuhakikisha walemavu wa aina zote wanakopesheka kupitia halmashauri wanazoishi kwa kuunda vikundi ama hata mmoja mmojahivyo niwaombe kuweza kuchangamkia fursa hizo ambazo zitawakwamua kiuchumi” Alisema Mariam Ulega Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake.

Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana zawadi

Mbali na kuwakabidhi mahitaji hayo Bi, Mariam Ulega amewataka walemavu hao kutembea kifua mbele kwani Rais Dkt Samia amekuwa ni nguzo kubwa kwa  watanzania wote na ndio mana amekiwa akisisitiza jinsia zote kuwajibika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa idara ya wanawake na watoto shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (shivyawata) Bi, Nasirya Ally  amempongdza Mariam Ulega kwa jinsi amavyo amekuwa msaada kwao na hasa kwenye utoaji wa misaada mbalimbali ambayo amekuwa akiwapatia wao.

Aidha amemtaka kuendelea na moyo huo huo na Mungu atamsaidia kwani Mungu anawapenda watu wanawasaidia wenzao.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments