Na Shushu Joel, Mlandizi
![]() |
| Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu akiwa na wanafunzi wa shule ya wasichana Ruvu sekondari mara baada ya kuwapa somo la ukatili ( NA SHUSHU JOEL) |
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu amelaani vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikosa hofu ya Mungu.
Akizungumza na Wanafunzi wa shule ya sekondari Ruvu Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo alisema kuwa kuna mambo maovu na ya kumchukiza Mungu yanazidi kufanyika nchini hivyo ni vyema nanyi kama watoto wetu tunapaswa kuwaeleza ili muweze kuwa mabarozi wakubwa wa kupinga vitendo hivyo.
" Kuna hali ya uchafu inaendelea kwa Wanaume kwa wanaume kuingiliana kimwili na Wanawake kwa wanawake nao wanaingiliana kitu ambacho hata wanyama hawafanyi" Mwenyekiti Vulu.
Aidha amewataka wanafunzi hao kutakuwa na tamaa ya aina yoyote ile kwani mambo hayo yapo tu na watayaacha hivyo amewasisitiza kuendelea kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwathibitishia wazazi na walezi wao kuwa hajaenda shule kuchezq bali kutafuta maarifa.
" Kuna Wamama wanatembea na watoto wao wa kuzaa na kuna Wababa wanatembea na mabinti zao wa kuzaa hii ni laana kubwa hivyo watoto wasemeni wazazi hao ili wachukuliwe hatua kali za kisheri" Vulu.
Aidha Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Pwani aliongeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anawapenda sana watanzania ndio maana amekuwa mstali wa mbele kukemea vitendo hivyo vya ajabu hapa nchini.
Naye Fatuma Mkonga ambaye ni mjumbe wa jumuiya amewataka wanafunzi kutimiza wajibu wao kama vile ilivyokusudiwa kwao.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefuta ada kwa kusudi la kuwataka wanafunzi waweze kusoma kwa bidii na kuwezq kuendelea na elimu za juu kwenye vyuo mbalimbali ili baadae watoto hao waweze kuja kuwa viongozi wa kesho katika Taifa hili.
MWISHO

0 Comments