STANBANK WAJITOA KUPAMBANA NA JANGA LA CHANGAMOTO LA UKOSEKANAJI MADAWATI

 Na Shushu Joel

Bank ya Stanbic  ya jijini Dar es salam imetoa msaada wa madati 100 yatakayotumika kwa wanafunzi 300 kati ya 500 waliokuwa wakikaa chini katika shule ya msingi Kiromo wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Meneja ya Bank ya Stanbek akiongozana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Bagamoyo na wawakilishi wa wanafunzi wakipokea madawati ( NA SHUSHU JOEL)

Akikabidhi msaada huo kwa Uongozi wa wilaya ya Bagamoyo Meneja  wa Bank hiyo Tawi la Center Bw Richard Chenga alisema hatua hiyo ni muelendelezo wao wa kampeni ya kusaidia madawati mashuleni.

Alisema  walipata taarifa ya upungufu mkubwa wa madawati na hivyo kuamua kutoa msaada huo ili kupunguza sehemu ya changamoto. 

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo  Bibi Flora Mlowe alisema wanagunzi zaidi ya mia tano walikuwa wakikaa chini kwa kukosa madawati.


"Wanafunzi wetu walikuwa wakigombania kukaa katika madawati kutokana na upungufu mkubwa na yule mwenye nguvu ndio upata nafasi:


Alisema wanamshukuru Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa kwa kusikia kiio chao na kuwatafuta Stanbic Bank ili kusaidia kutatua changamoto  hiyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa aliishukuru Bank hiyo kwa msaada huo mkubwa.


Alisema ni kweli kuna changamoto kubwa ya madawati lakini pia kuna changamoto ya ukatili kwa watoto hali inayosababisha wengi kukosa elimu.


Aliiomba Serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wote wanaosababisha  vitendo vya mimba na utoro mashueni.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bibi aliishukuru Bank  hiyo na kuiomba kusaidia maeneo mengine ndani ya wilaya hiyo kwani changamoto ni kubwa licha  ya Serikali ya awamu ya sita kutatua changamoto mbalimbali

MWISHO

Post a Comment

0 Comments