WANAWAKE RUFIJI, KIBITI NA MKURANGA WAHAMASIKA MIAKA MIWILI YA DKT SAMIA MADARAKANI.

 Na Shushu Joel  Pwani


WANAWAKE wa Mkoa wa Pwani kutokea wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 19/ 03/ 2023 katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo wanakwenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarani .

Viongozi wa UWT Mkoa wa Pwani wakihamasisha wanawake wenzao kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 19 huku wakiwa na picha 


Wakizungumza kwa wakati tofauti tofauti kamati ya utekelezaji ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani ikiongozwa na katibu wa jumuiya hiyo Bi,  Fatma Ndee alisema kuwa tumeamua kufanya hamasa kubwa kwa wananchi wenzetu iliwawwze  kumsikiliza Dkt Samia Suluhu Hassan kwa. 


Ndee alisema kuwa wameamua kufanya hamasa hiyo katika wilaya hizo ili kila mmoja aweze kufika katika sherehe hizo na kusikia kile kilichofanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa watanzania wote.


Ziara hiyo ya kutoa hamasa kwa wananchi hao imeambatana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutokea Mkoa wa Pwani Bi Mariam Ulega, Fatma Mkoga  Mjumbe wa wa Baraza la utekelezaji Mkoa na Catherine Sebastian mjumbe wa Baraza la utekelezaji ambao wote wamemsemea Rais jinsi anavyoupiga mwingi kwa Taifa letu.


Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Rufiji  Rehema Mlawa  ameipongeza kamati hiyo ya Mkoa kwa ubunifu wa kutoa hamasa kwa jamii ili kuweza kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya uhuru.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Tatu Mkumba  wilaya ya Kibiti ameihakikishia kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoa kuwa wao wameshajipanga kwa safari ya kwenda kumsikiliza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hiyo siku ya tarehe 19.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments