MWENYEKITI UWT KIBAHA VIJIJINI AWATAKA WANAFUNZI KUZINGATIA MASOMO.

 Na Shushu Joel, Mlandizi 

MWENYEKITI wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Kibaha vijijini Mkoani Pwani Bi, Leila Hamoud Jumaa amewataka wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kuongeza juhudi katikab masomo yao ili waweze kufaulu kwa kiwango cha juu.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kibaha vijijini akiteta jambo na mmoja wa Wanafunzi wa Ruvu sekondari mara baada ya kikao ( NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipotembelea shule ya sekondri ya Wasichana ya Ruvu ambapo aliwakumbusha kila mmoja kuweza kutambua wajibu wake wa uwepo shuleni.


" kila mmoja hapa mlipo anandoto zake ambazo amejiwekea katika masomo yake hivyo niwatake wanangu kila mmoja wenu asome  kwa bidii ili akamilishe ndoto zake" Leila Jumaa.


Aidha Mwenyekiti huyo wa UWT amewataka wanafunzi hao kuepuka vitendo vya kushawishiwa na vijana ili waweze kutembea nao kataeeni mambo hayo kwani mtaalibu malengo yenu.


Kwa upande wake Mwajuma Ibrahimu ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili amempongeza Mwenyekiti wa UWT kwa kuonyesha upendo wa dhati kwa sie watoto wake kwa kututembelea shuleni na kutupatia elimu ya mtaani.


Aidha niwaombe wanafunzi wenzangu kuweza kuzingatia maneno yaliyotolewa na Mama yetu ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Kibaha Vijijini. 

MWISHO

Post a Comment

0 Comments