Na Shushu Joel, Mkuranaga
JUMUIYA ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Abdallah imepigwa msasa ili kila mmoja aweze kutambua mwanzo na mwisho wa mipaka yake katika utendaji wa kazi.
![]() |
| Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Mkuranga Juma Mahege akifuatilia mafunzo kwa makini ( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo mwenyekiti wa Wazazi wilaya hiyo Ndg Juma Mahege alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo ili kuwasaidia viongozi wa jumuiya na wale baadhi wa chama ambao wengi ni wapya katika uongozi.
Aliongeza kuwa mafunzo waliyoyapata viongozi wenzangu wa kata yanakwenda kuwafanya kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kwa uhakika.
Aidha Mwenyekiti Mahege amewapongeza viongozi wa jumuiya hiyo kwa kujitokeza kwa wingi ili kuja kujifunza mafunzo ya uongozi na pia kuzidi kujijua kanuni za Chama Cha Mapinduzi zaidi.
Mbali na mafunzo hayo Mwenyekiti huyo amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kwa jinsi ambavyo qmbavyo amekuwa kiongozi wa mfano katika wilaya kwa kuhakikisha viongozi wa chama wanakuwa na uelewa katika utendaji kazi zao.
Aidha amewataka viongozi hao kwenda kupambana na mambo ya ovyo yanayoendelea katika jamii zetu kwa watoto kubakwa na wa kiume kulawitiwa kwa nguvu zao zote ili kuweza kutokomeza jambo hilo.
Naye Farida Kafuku ambaye ni katibu wa kata ya mipeko kutokea jumuiya hiyo ya wazazi amemponhgeza Mwenyekiti wa wilaya hiyo kwa kuwapatia mafunzo ambayo yanakwenda kuwafanya kuwa viongozi bora na wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi wote katika kata zao.
Aidha amehakikisha kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia vile ilivyokusudiwa ili kuweza kujenga jumuiya hiyo.
MWISHO


0 Comments