NA MWANDISHI WETU
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Machi 12, 2023 amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain wakati Kauli mbiu mkutano huo ni “Kukuza amani na kujenga Jamii Jumuishi yenye kuvumiliana”.
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain
Dkt. Tulia amezungumzia
kuhusu kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na
Bunge katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa Wananchi wake
pamoja na kuheshimu Maazimio ya Kimataifa katika kulinda na kudumisha amani
Duniani.
Wakati huohuo, Dkt. Tulia
amewasilisha hoja ya dharura kwa niaba ya kundi hilo kuchagiza kuundwa kwa mfuko
wa maafa Duniani kwa ajili ya kusaidia Nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili
na mabadiliko ya tabianchi.
Pamoja na hoja hii, hoja
zingine nne ziliwasilishwa na Mataifa mbalimbali. Hoja hizi zinatarajiwa
kupigiwa kura ya maamuzi hapo baadae ili Umoja huo kupitisha hoja moja ya
dharura ambayo itajadiliwa, kuboreshwa na hatimaye kutengeneza azimio la
Mkutano huo.
0 Comments