ALHAJI MANSOUR AWAKUTANISHA WANA PWANI PAMOJA KWA IFTARI.

Na Shushu Joel

Mwakilishi wa Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mansour Ndugu Mohamed Sheikh Mwenye tisheti Nyeusi akikabidhi futari kwa viongozi wa CCM Mkoa( NA  SHUSHU JOEL)

MJUMBE wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndugu Mussa Mansour amegawa futari kwa viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa ngazi za kata, wilaya na Mkoa.


Akizungumza wakati wa zoezi hilo la ugawaji futari  hiyo mwakilishi wa Mjumbe  huyo ndugu Mohamed Sheikh alisema kuwa futari iligawia ni kuonyesha upendo kwa watu wenzake kama vinavyosema vitabu vya dini.

Aliongeza kuwa Alhaji Mansour amewataka wananchi kuendelea kuwa na umoja na upendo wa dhati kwa Taifa letu ili kizazi kijacho kiweze kutambua thamani ya nchi yetu.

Aidha Mwakilishi huyo wa Alhaji Mansour amewataka wazazi na walezi kuendelea kuungana kwa pamoja ili kuweza kupinga vitendo vya ovyo vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa kuwalawiti watoto na hata kukemea vitendo vya ushoga ambavyo Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa akivikemea sana.

Pia amewataka wananchi wa Mkoa wa Pwani kuendelea kuwaombea viongozi wetu ambao wamekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tifa letu ili waweze kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.


“Tuendelee kuwa na moyo wa upendo na wa kujitoa kama ambao amekuwa akiufanya Alhaji Mansour kwani ni mtu ambaye ni mwenye hofu ya Mungu” Alisema Mohamed

Naye Amina Makona ambaye ni  katibu wa vijana (UVCCM) wilaya ya Kibaha amempongeza Alhaji Mansour kwa moyo wake wa upendo aliounyesha kwa viongozi mbalimbali wa CCM.

Aidha amewataka viongozi wengine kuiga mazuri ambayo yamekuwa yakifanywa na mjumbe huyo wa kamati ya siasa Mkoa.

MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments