NA MWANDISHI WETU SINGIDA
Vijana wenye ujuzi mbalimbali Mkoani Singida Wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa miradi ya Serikali ya Ujenzi wa vyumba 102 vya madarasa na matundu 116 ya Vyoo maeneo mbalimbali Mkoani hapo kupitia mradi wa BOOST Kama fursa ya kujipatia ajira.
![]() |
| Afisa Vijana Mkoa wa Singida akifafanua jambo mbele ya vijana waliojitokeza kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa huo |
Kauli hiyo imetolewa na hivi karibuni na Afisa vijana wa Mkoa huo Fredrick Ndahani alipokutana na makundi ya vijana hao katika ukumbi wa mikutano wa Social RC Mission ulioko mjini Singida.
Afisa Vijana huyo amesema serikali imetoa Jumla ya Tsh Bilioni 9.024 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa matundu ya vyoo nyumba za walimu na ukarabati wa shule hivyo vijana watumie miradi hiyo kuonesha uwezo wao.
Ndahani akiwa Katika semina hiyo amesema Vijana wasisubiri fursa ziwafuate bali wazitafute zilipo kwa kuwa hawezi kujulikana mtu bila ya kujitangaza huku akiwasisitiza kutumia fursa zinazotolewa na Serikali.
"Ombeni kazi Katika miradi hiyo kwakuwa hakuna mtu atakaye jua kuwa fulani ni fundi bila ya wewe kutoka na kuonesha ujuzi ulionao Kijana" alisema Ndahani
Aidha Ndahani amewaeleza Vijana kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kutoa mikopo kwa Vijana yenye masharti nafuu na ambapo mpaka jumla ya Shilingi 118,675,000 zimetolewa kwa vikundi vya vijana katika Mkoa wa Singida.
Saimon Mandela ameshukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutenga muda wa kuongea na Vijana kwani Vijana wengi hawajuwi fursa zinazotolewa na Serikali pamoja na Miradi inayoletwa ndani ya Mkoa ambayo Vijana wanaweza kuomba na kupatiwa ajira
na ukarabati wa maradasa ya Elimu ya Awali

0 Comments