TEMEKE WAANZA MAANDALIZI YA WAZAZI CUP

Na Shushu Joel, Temeke

WILAYA ya Temeke iliyoko Jiji la Dar es Salaam imeanza mikakati ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya Wazazi Cup yanayotarajia kuanza hivi karibuni ambayo yatafanyika katika uwanja wa uhuru maarufu shamba la Bibi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke Khamis Slim akifafanua jambo mbele ya makatibu kata(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza kwenye kikao kazi cha maandalizi ya michuano hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Wilaya hiyo ya Temeke Khamis Slim alisema kuwa tumeamua kuanza maandalizi ya michuano hiyo mapema kwa kusudi la kubeba ubingwa.

 

Alisema kuwa wilaya ya Temeke ni wilaya pekee yenye viwanja vya mpira vya kisasa ikiwemo uwanja wa Uhuru na kile cha Mkapa maarufu Lupaso hivyo kutokana na uwepo wa viwanja hivyo ni lazima ubingwa uwe kwetu na hiki ndicho kilichopelekea kuanza kwa maandalizi mapema.

“ Nimekutana na makatibu wa wazazi wa kata zote za wilaya ya Temeke ili kuweza kuanzisha mashindano madogo ndani ya kata zao ili waweze kuchagua vijana wataokao weza kuunda timu mbili za jimbo ambazo zitakwenda kushindana na timu za wilaya zingine za Mkoa wa Dar es Salaam” Alisema Slim

Aidha Mwenyekiti huyo wa Wazazi amewataka vijana wote watakaopata nafasi ya kuchaguliwa na kuunda timu za wilaya ya Temeke wahakikishae wanatumia nafasi hii kuonyesha kipaji chao ili waweze kufika mbali kwani michezo ni ajira.

Alisema kuwa wilaya ya Temeke ndio wilaya pekee hapa nchini inayomiliki viwanja viwili vya viwanja vya mpira vya kisasa hivyo ubingwa ni laima uje temeke kutokana na vipaji lukuki vilivyo jaa kwenye wilaya hiyo.

Naye katibu kata ya Mbagala Mtupa  alisema kuwa kuanzishwa kwa Wazazi Cup kunakwenda kufungua milango kwa vijana wa wilaya yetu kuweza kujitangaza kupitia vipaji vyao hivyo wanatakiwa kupambana ili kuonekana kama ilivyokuwa kwa vijana wengine ndani nan je ya nchi ambao wametumia fursa za michozo kuonyesha vipajai vyao na hata kutimiza ndoto zao.


Hivyo amesema kuwa jumuiya ya Wazazi imekuja na wazo zuri ambalo linakwenda kuwasaidia vijana wa nchi hii pasipo na wasiwasi wowote ule.

 

Naye Kaimu mratibu wa michezo wa mashindano hayo Bi,Ivonn Elias amehaidi kuwasaidia vijana hao kwa lengo la kutimiza ndoto nzao za kucheza mpira wa miguu.

Aidha amesisitiza juu ya nidhamu kwa wachezaji kwani nidhamu ndio kila kitu katika michezo hivyo kama mtu hana nidhamu ni bora tu akaacha kucheza mpira

MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments