Na Shushu Joel
MJUMBE wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndugu Mussa Mansour ameshiriki katika ibada ya Umra Makka.

Mussa Mansour mwenye kibegi akiwa katika sambamba na waumini mbalimbali katika ibada ya umra akipata Dua( na shushu joel)
Akizungumza
kwa njia ya simu Mansour alisema kuwa ni vyema kila mmoja wetu akawa karibu na
MOLA kwani dunia ni mapito hivyo ni vyema kutengeneza amana kubwa kwa muumba
wetu.
Alisema kuwa
matendo mema ni sadaka kubwa na pia tuendelee kumuomba ALLAH aweze kuzikubali Dua zetu ili sisi wote
kwa pamoja tuweze kuwa na mwisho mwema.
“Hakika hii
Dunia ni mapito na ina mazuri mengi sana na kuna kila aina ya safari ambazo
zitakupeleka katika kila pembe uitakayo lakini kona iliyo bora ni ile
itakayokuweka karibu Zaidi na MOLA wako” Alisema Mansour
Aidha
aliongeza kuwa ametumia nafasi hiyo kuwaombea watanzania wote ili nchi yetu
iendelee kuwa na neema Zaidi.
0 Comments