Na Shushu Joel, Kibaha
MJUMBE wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour amewataka wana Chana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani kuwa na umoja na upendo wao kwa wao pia na kwa viongozi wao.
![]() |
| Alhaji Mussa Mansour akitoa somo la upenda kwa wana chama na viongozi wa ccm kibaha( NA SHUSHU JOEL) |
Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na viongozi wa chama hizo ngazi ya matawi na kata waliokutana kwenye mafunzo katika ukumbi wa Chuo cha uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha.
Mansour alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi ni urithi kutoka kwa waasisi wetu ambao ni Hayati Nyerere na Karume ambao walipendana na ndio maana wakatengeneza umoja ambao mpaka leo kila mtanzania anajivunia.
" Sisi viongozi na Wanachama wa kawaida tukizidisha upendo na umoja chama chetu kitaendelea kuwa bora zaidi ya hapa tulipo sasa hivyo kila mmoja ampende mwenzeka" Alisema Alhaji Mansour
Aidha Alhaji Mansour amewakumbusha wana CCM wote Mkoa wa Pwani kuendelea kukisemea Chama kwa yale mazuri yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani mengi yamefanyika hivyo kila mwana CCM anawajibu wa kusema juu ya chama .
Mbali na hayo Alhaji Mansour amefungua milango kwa wana CCM wote wanaotaka kumwalika katika kujenga chama kwani hii itasaidia kuyatangaza yote yaliyofanyika katika Mkoa wa Pwani.
" Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya maendeleo mengi na makubwa katika Mkoa wa Pwani ila wana CCM hawayatangazi sijui kwa nini niwaombe muyaseme ili jamii ijue jinsi gani chama chetu kimekuwa kikifanya makubwa" Alisema Alhaji Mansour
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo ya Kibaha Mji Mwajuma Nyamka amempongeza Mjumbe huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa akishiriki katika mambo mbalimbali ya Chama.
MWISHO



0 Comments