"SERIKALI ITAZIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA BARABARA NA UMEME" KOKA

 Na Shushu joel, kibaha

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Slyvester Koka amewatoa hofu wananchi wahilo kuwa serikali inazidi kuchakata ili iweze kutoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara za Kibaha Mji na kuendelea kusambaza umeme kwa baadhi ya maeneo ambayo bado hawajafikiwa na huduma hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya uongozi kwa viongozi mbalimbali wa matawi na kata yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere, Koka alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo bado yanachangamoto lakini yanazidi kufanyiwa kazi

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji akifafanua jambo mbele ya viongozi wa CCM

Alisema kuwa ni ngumu kumaliza changamoto zote kwa pamoja lakini naamini changamoto hizo zina kwenda kumalizika kipindi hiki cha uongozi wa Rais wetu wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya kibaha Mjini Mwajuma Nyamka alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo ya Kibaha Mji yamekuwa na changamoto ya kutokupitika kwa urahisi kutokana na miundombinu kuwa mibovu.


Aidha amemtaka Mbunge Koka kuhakikishia analivalia njuga jambo hilo ili papitike kwa urahisi na wananchi waweze kupita kwa urahisi na wafanye kazi zao za kujiingizia kipato kwa urahisi

MWISHO

Post a Comment

0 Comments