Na Shushu Joel, Kibaha
MJUMBE wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour amewataka wananchi wote wa wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuweza kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuulaki Mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuingia kesho katika wilaya hiyo
![]() |
| Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour akiwa ameshika mwenge wa uhuru ( na shushu joel) |
Alhaji Mansour alisema kuwa Mwenge ni tunu kubwa tuliyoachiwa na waasisi wetu ambao ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Karume hivyo wana Kibaha tumiminike kuupokea na kuukimbiza katika miradi ambayo Mwenge huo unakwenda kupita kuzindua miradi mbalimbali.
Alisema kuwa kibaha imekuwa na miradi mingi ambayo imekamilika na mingine mingi inazidi kutekelezeka kupitia serikali kuu na ile ya Halmashauri pamoja na miradi ya wadau mbalimbali.
Aidha Alhaji Mansour amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa miradi iliyopo Kibaha hii inaonyesha jinsi gani Rais wetu amekuwa mtekelezaji mkubwa wa miradi.
Aidha Alhaji Mansour amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita katika uletaji wa maendeleo.
Naye Abubakar Nombo amempongeza Mjumbe huyo wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhamasisha wananchi wanatako sehumu mbalimbali za kanda .
Aidha amewataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kujionea jinsi Mwenge wa Uhuru unavyozindua miradi mbalimbali.
MWISHO

0 Comments