MWENGE KUTEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI TRION 4.4 PWANI .

 Na Shushu Joel ,Pwani.

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amepokea Mwenge wa uhuru ukitokea Mkoa wa Morogoro katika halmashauri ya Chalinze  Mkoani humo

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akikabidhiwa Mwenge na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa Kunenge alisema kuwa miradi hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa uhuru ni ile ya serikali kuu, halmashauri na wadau mbalimbali ambayo kwa ujumla inafikia 99


Alisema kuwa miradi yote ni  utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo Mwenyekiti wake wa Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha kwa wasaidizi wake kwa kusudi la kuwapatia huduma wananchi.


" Mwenge huu unakwenda kuwa kielelezo kikubwa kwa wanqnchi kwa kutambua kile kinachofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa watanzania" Alisema Kunenge. 


Kwa upande wake kiongozi wa  mbio za mwenge kitaifa Abdala Shaib Kaim amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa miradi hukuvakisisitiza wao wako tayari kukagua na kuzindua miradi hiyo .


Aidha amewapongeza kwa hamasa kubwa wanayoifanya kwa wananchi hasa kujitokeza kwenye mwenge unaopita na kukagua miradi katika halmashauri ya Chalinze. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments