Na Shushu Joel, Dar es Salaam
MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa Ndugu Abubakari Jafo amemsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kumalizika kwa wakati na inawanufaisha wananchi.
![]() |
Abubakar Jafo akiwa katika picha ndani ya Mkutano huo( NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza mara baada ya usomaji wa utekelezaji wa ilani wa kata ya Vituka ambapo imeonyesha ni jinsi gani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kinara katika utekelezaji wa maendeleo kwa jamii.
Alisema kuwa kuna miradi mingi sana nchini inazidi kumaliziwa na mipya inazidi kutekelezeka na hii yote inaonyesha ni jinsi gani Mwenyekiti wetu wa CCM anavyopambana na kumaliza changamoto ambazo zinawakabili watanzania.
Aidha Jafo amempongeza Diwani wa kata hiyo kwa uwasilshaji wa utekelezaji uliojaa matumaini makubwa katika sekta zote ikiwemo Afya, Elimu, Maji na miundombinu ikizidi kuongezeka siku hadi siku.
Mbali na hilo Jafo ameitaka jamii kuwa walinzi wa miradi ya maendeleo kwani tulitaabika sana wakati miradi hiyo haikuwepo hivyo sasa ni lazima tutunze miradi yetu ili watoto na wajukuu wetu waweze kuitumia miradi hiyo.
Naye Abel Mkengwa ambaye ni Mwenyekiti wa Wazazi CCM kata hiyo amemsifu diwani kwa usimamizi na utekelezaji wa Ilani ya chama.
Aidha amemtaka kuendelea kupiga kazi kwani wananchi wanahitaji maendeleo na si kitu kingine.
MWISHO
0 Comments