Na Shushu Joel, Mkuranga
WANANCHI wa kata ya Mgawa wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wamesema kuwa wanadeni kubwa wanalodaiwa na Mbunge wao wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.
![]() |
| Salu Bofu akisema neno kwa Mwenyekiti jinsi walivyofanyiwa na Mbunge Ulega( NA SHUSHU JOEL) |
Hayo wamesema walipokuwa kwenye kikao na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Mkuranga Ndugu Juma Mahege kwenye moja ya mkutano yake iliyofanyika katika kata hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho mmoja wa wazee maarufu Ndugu Salum Bofu alisema kuwa kata yetu ya Mgawa miaka ya nyuma ilikuwa haitamaniki kwenye miradi ya maendeleo lakini kipindi hiki kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali na hii yote inatokana na ushupavu wa Mbunge wetu Mhe. Abdallah Ulega umekuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika kata hiyo na Mkuranga kwa ujumla.
Aidha Bofu alisema kuwa miaka wao wanakuwa kulikuwa hakuna hata mawasiliano kutokana na kutokuwepo kwa mtandao lakini sasa hivi uchumi umezidi kukua kutokana na kufunguka kwa barabara zinzoingia katika kata hiyo kutokea sehemu zingine za nje ya kata yetu.
Alisema kuwa kutokana na hali hii kubwa ya maendeleo inayofanywa na Mbunge Ulega kwa niaba ya wote tunasema tunadaiwa mambo mengi na mbunge kwàni ametafuna mifupa iliyowashinda.
Naye Fatuma Mbwera ( 72) alisema kuwa wananchi wa kata ya Mgawa tuna deni kubwa la kumlipa Mhe. Ulega kutokana na jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa wa maendeleo katka kata hiyo na jimbo kwa kwa ujumla .
Aidha amewakumbusha wananchi wa kata hiyo kukumbuka kule waliķo toka mpaka sasa hapa tulipo kwani maendeleo mengi yamefanyika chini ya Mbunge Ulega.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Mkuranga Juma Mahege amewasifu wananchi kwa kuwa na kumbukumbu ya walikotoka na walipo sasa.

0 Comments