MWENYEKITI WA WAZAZI BAGAMOYO ASISITIZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI.

 Na Shushu Joel,  Bagamoyo 

Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa akisisitiza jambokwa viongozinwa matawi na kata (NA SHUSHU JOEL)

MWENYEKITI wa jumuiya ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Abubakari Mlawa amewataka viongozi wa matawi na kata kuwa wazazi na uwajibikaji kwa wananchi ili wazidi kuaminika katika utendaji wao.


Rai hiyo ameitoa kwenye Mbio za Bendera zinazoendelea wilayani humo ambazo mbio hizo zinalenga kufufua uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uwajibikaji kwa viongozi mbalimbali waliopewa dhamana na Chama hicho.


Mlawa alisema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa viongozi wengi wa Chama na Serikali wamekuwa wakifanya maamuzi bila kuwashilikisha wananchi.


Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ili tufanikiwe katika uongozi ni lazima tuwashilikishe wale tunaowaongoza ambao ni wananchi.


" Msiache kuwashirikisha wananchi katika ufanikishaji wa maendeleo kwa jamii kwani mkiwashirikisha mnaondoa maswali kwa jamii inayowazunguka" Alisema Mwenyekiti wa Wazazi wilaya hiyo Ndg Mlawa.


Naye Diwani wa kata ya Kerege Said Ngatipula amemwakikishia Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo kuwa wanakwenda kuwa wawazi kwa wananchi ili wajue kile wanachofanyiwa na viongozi wao.


Aidha Ngatipula aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita imekuwa msaada mkubwa wa maendeleo kwa kata hiyo kwani wamefanikiwa kupata fedha zaidi ya milion 800 za miradi ya maendeleo. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo Abdulsharifu Zahoro  amesifu Mbio za  Bendera zinazoendelea wilaya humo kwani zimekuwa zikifufua uhai wa Chama.


Aidha amewasifu wajumbe wa kamati ya siasa wilaya kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakitoa elimu kwa viongozi wa matawi na kata .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments