WAZAZI PWANI YAZIDI KUCHANUA

Na Shushu Joel, Mkuranaga 

Katibu wa Wazazi Mkoa wa Pwani Elisante Msuya akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika ofisi za ccm kata ya Mwandege ( NA SHUSHU JOEL)



JUMUIYA ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Pwani imezidi kupasua anga katika mwendelezo wa ziara zake ambazo zinaendelea katka wilaya ya Mkuranga. 


Akizungumza na Viongozi wa jumuiya kuanzia ngazi ya matawi hadi kata katibu wa Wazazi Mkoa wa Pwani Ndugu  Elisante Msuya alisema kuwa wameamua kuwafuata viongozi wa matawi na kata kwani huko ndio kuna changamoto mbalimbali.


Aidha amewapongeza wananchi wanaojitokeza kutoa kero zao mbele ya viongozi wa jumuiya hiyo na wamekuwa wakitatuliwa changamoto zao.


Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya  Mwandege Hemed Kiluke  amempongeza katibu wa Wazazi wa Mkoa na timu yake kwa jinsi ambavyo wanafanya kazi ya kutembea kata zaidi ya tano kwa mkuranga kwa kugawana na kuzungumza na wanachama .


Alisema kuwa wazo hili ni zuri sana kwa jumuiya kwani tunakwenda kuimalisha chama na jumuiya kwa ujumla.

Aidha aliongeza kuwa na sie chama tumeamua kulichukua wazo lililofanywa na wazazi ili nasi tulifanye kwenye kata kwa kuwatembelea wananchi kila kijiji.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments