Na Shushu Joel, Kibaha.
MJUMBE wa baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi Mariam Ulega amewataka Wanawake wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kudumisha mshikamano ndani ya Jumuiya na nje ili kuweza kusaidia jamii yetu.
![]() |
| Mariam Ulega Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa akifafanua jambo |
Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na Wanawake wa kata ya Kibaha kwenye Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
Alisema kuwa Wanawake tunapokuwa na Mshikamano tutalisaidia Taifa letu kwenye nyanja mbalimbali na hasa za ukuaji wa uchumi wetu.
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha maendeleo ya Taifa letu yanazidi kukua.
"Kwa kweli Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa mfano na mwenye kuigwa katika Taifa letu na Dunia kwa ujumla na hii ni kutokana na utendaji wake wa kazi kwa Watanzania" Alisema Mjumbe wa baraza la UWT Bi, Mariam Ulega.
Pia katika Mkutano huo Mjumbe huyo amewaunga mkono wanawake wa kata hiyo kwa kuwachangia kiasi cha Shilingi Milioni mbili ili ziweze kuwasaidia katika kukuza mtaji wao.
Aidha awasisitiza viongozi mbalimbali wa Jumuiya kuendelea kushuka chini kwa jamii ili kusikiliza changamoto zinazowakabili kama vile wanavyofanya viongozi wetu wa kitaifa Mama Chatanda na Makamu wake Mama Shomari.
"Rais wetu kafanya mambo mengi na ya kuonekana kwa Watanzania hivyo hatuma wasiwasi na kura kwani mengi yanaonekana ambayo Mama Samia Suluhu Hassan ameyafanya kwa ufanisi wa hali ya juu" Alisema Bi, Mariam Ulega
Naye Mwenyekiti wa UWT kata ya Kibaha Mama Mahelo amemsifu Mjumbe wa baraza la UWT Taifa kwa maneno yenye hekima kwa Wanawake wa kibaha na Pwani kwa ujumla.
MWISHO


0 Comments