NA MWANDISHI WETU
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Lawrence Peter Tsingay, amekabidhi seti moja ya jezi na mpira mmoja kwa vijana wa bodaboda wa Mdaula kata ya Bwilingu
Aidha alisema kuwa ni vyema vijana kujiepusha na mambo yasiofaa na kushiriki kwenye michezo kwani michezo inaondoa mambo mengi ya kishawishi
Pia aliongeza kuwa ni vyema kuwaunga mkono viongozi waliotokana na Chama Cha Mapinduzi, diwani, mbunge na rais. "Shikeni michezo kwenye muda wenu wa ziada, itawasaidia kujiepusha na mambo yasiyofaa kwakuwa nyinyi bado vijana damu zenu zinachemka.
Aidha aliongeza kuwa ni vizuri Tuwaunge mkono viongozi wanaotokana na CCM kuanzia diwani wetu, Mh mbunge Ridhiwani Kikwete kwa uchapa kazi wake kama mnavuojionea miradi mikubwa kutokana na jitihada zake lakini pia amesisitiza tumuunge mkono Mh Rais, Dkt Samia Suluhu Hasani."
Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa Boda boda Huseein Ally alisema kuwa mjumbe huyo ni mfano wa kuigwa kwa vijana kutokana na moyo wake wa kujitoa kwa vijana na jamii kwa ujumlahivyo amewataka wengine kuiga mfano huo.
MWISHO
0 Comments