MWENYEKITI UVCCM ILALA ATOA SOMA KWA VIJANA

 Na Shushu Joel, Ilana

Mwenyekiti wa UVCCM Juma Mizungu akifafanua jambo kwa vijana ( NA SHUSHU JOEL)


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam Juma Mizungu amewapa somo vijana wa Jumuiya hiyo ili kuondokana  na utegemezi na badala yake kila mmoja wake kuweza kukwamuka kiuchumi. 


Somo hilo amelitoa alipokuwa akizungumza kwenye Baraza la vijana kata ya Kitunda.

Aliwataka vijana kujitambua na kuachana na tabia za miemuko isiyokuwa na tija wala mwelekeo kwao na badala yake amewasihi kuweza kuungana na kuwa wamoja .


 Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya ya Ilala amewakumbusha vijana kuendelea kumsemea mazuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi ili waweze kuona kile kilichofanyika na kinachoendelea kufanywa na Rais huyo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kata hiyo amemsifu Mwenyekiti wa wilaya kwa jinsi ambavyo amezidi kuwa kiongozi mwenye maono ya mbali kwa jumuiya hiyo.


Aidha amewataka vijana wenzake kuiga mienendo mizuri inayofanywa na kiongozi huyo wa wilaya .


MWISHO

Post a Comment

0 Comments