Na Calvin Minja-NIDA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanzisha operesheni maalum ya kuwasaka na kushughulikia watu wanao walaghai wananchi kuwa ni watumishi wa NIDA kwa lengo la kuwatapeli na kujipatia fedha isivyo halali.
Operesheni
hiyo iliyoafanyika nchi nzima imefanikiwa
kukamata watu kadhaa wanaojifanya ni Maafisa wa NIDA na wanaochapisha Nakala
Tepe (Online Copy) wakiwemo wafanyabiashara wa maduka ya Steshenari.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa mkutano na vyombo vya habari, Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano wa NIDA, Geofrey Tengeneza amesema Alhamis Tarehe 14/09/2023
wamefanikiwa kumkamata mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Gibson Buberwa
aliyejifanya ni Mratibu wa NIDA kutoka Ilala, Dar es Salaam.
Mtu
huyo alikamatwa na maafisa wa NIDA kwa kushirikiana na jeshi la polisi mtaa wa
Majengo, Kata ya Vingunguti akiwa na fomu za Usajili wa watu zinazotumiwa na
NIDA baada ya kuwekewa mtego na hatimaye kunaswa.
Amesema
mtu huyo alikuwa akitumia fomu hizo za NIDA kuwasajili watu akiwaaminisha kuwa
watapata Vitambulisho vya Taifa na kuwataka kutoa malipo ya shilingi 5,000 kwa
kila mtu. Ametoa onyo kwa watu ambao si watumishi wa NIDA kuacha mara moja kujifanya
ni maafisa wa NIDA na kutapeli wananchi.
Kuhusu
huduma ya Online Copy Tengeneza amesema NIDA ilikwisha sitisha huduma ya Nakala
Tepe (Online Copy) toka mwaka 2019 na kwamba yeyote anyetangaza kutoa huduma
hiyo ni mhalifu na akifahamika atachukuliwa hatuka kali za kisheria. Amewataka wananchi
kuendelea kutumia Namba zao Utambulisho hadi pale watakapopata vitambulisho.
“Tunashukuru
kwa ushirikiano tunaupata kutoka Maafisa wa Serikali za Kijiji/Mtaa pia tunatoa
wito kwa mtu mwenye taarifa juu ya matapeli aweze kufahamisha Jeshi la Polisi
au awasilishe kwenye Ofisi za NIDA za Wilaya.” alisema na kuongeza kuwa watu
wote wanaotumia jina la taasisi kufanya utapeli wanatakiwa kuacha mara moja, kwani
wanachokifanya ni kinyume cha sheria na wakamata na kuwachukulia hatua kali za
kisheria,
0 Comments