"SIJAWAI KUSIKIA CHANGAMOTO TOKA HOSPITAL YA KUMBUKUMBU CHARLES KULWA" DKT BITEKO

Na Shushu Joel, Bukombe 

MBUNGE wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko amekosho na utendaji kazi wa Hospital ya kumbukumbu ya Charles Kulwa katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika hospital hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.

Naibu Waziri Mkuu akikata utepe kwenye wodi Mpya iliyopo hospital ya Charles Kulwa(NA SHUSHU JOEL)

Hayo amesema alipokuwa akizindua wodi mpya katika Hospital hiyo ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa ambapo alisema kuwa Hospital hiyo tangu kuanzishwa kwake hapajawai kusikia wala kupokea changamoto yeyote  kutoka kwa wale wanaopatiwa matibabu.


Aliongeza kuwa hii inaonyesha jinsi gani wananchi wanapata huduma  bora na zenye kukizi mahitaji yao ya Afya.


Aidha amewataka watumishi wa serikali katika sekta ya Afya kuweza kuiga mzuri yanayopelekea Hospital hiyo ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa ili nasi serikali yatumike kwa kuwafurahisha wagonjwa wetu pale wanapofika kupatiwa huduma.


"Afya ni mtaji kwa kila mtu ni vyema sasa kila mmoja wetu akathamini afya yake kwa kujijengea mazoea ya kupima na kukagua mwili wake" Alisema Dkt Biteko 


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital hiyo Dr. Baraka Charles Kulwa amempongeza Naibu Waziri Mkuu kwa nasaha zake ambazo ni za kujenga na zenye mapenzi makubwa na Hospital ya kumbukumbu ya Charles Kulwa.

Aidha aliongeza kuwa siri kubwa ya mafanikio ni umoja na ushirikiano tulionao baina ya watumishi na viongozi.

Mbali na hayo Dr. Baraka amewapongeza wananchi wa Runzewe na majirani kwa ushauri mkubwa ambaonwamekuwa wakimpatiakwalengo la kuhakikisha hospitalinazidi kukua na kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa jamii.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments