Na Shushu Joel, Bukombe.
UPINZANI katika Jimbo la Bukombe Mkoani Geita umezidi kupukutika kwa kasi kutokana na maendeleo makubwa yanayofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko.
![]() |
| Dkt Dotto Biteko ambaye ni |
Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukombe Hassan Abdallah alisema kuwa Mhe. Biteko amefanikisha kurejesha heshima kubwa iliyopotea miaka iliyopita kutokana na wana CCM walio wengi kukimbilia upinzani lakini kutokana na kile kinachofanywa na Mbunge wengi wao wamerejesha kadi ndani ya CCM.
Aliongeza kuwa Maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hapa nchini kila mmoja amefumba mdomo kutokana na kutatuliwa kwa changamoto za wananchi kwa wakati pasipo kuangalia Chama.
" Jimbo la Bukombe lilizoeleka kwa mbunge kutawala awamu moja tu yaani miaka mitano lakini Mhe. Biteko ameuvunja mwiko huo" Alisema Hassan
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Bukombe (UWT) Bi Julieth Simon amempongeza Mbunge kwa juhudi zake za ufanikishaji wa maendeleo kwa wananchi jambo ambalo awali ilikuwa ni historia katika Jimbo letu la Bukombe.
Aidha amemwakikishia Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Wanawake wa Bukombe wanatambua thamani kubwa aliyowapatia Hivyo wao zawadi yake ataiona kwenye uchaguzi wa Serikali za Mtaa na uchaguzi Mkuu ujao.
"Wanawake wa Wilaya ya Bukombe tunajambo letu ambalo litaonekana kwenye uchaguzi ujao ambapo tumekubaliana tunachukua tunaweka kwa Dkt Samia" Alisema Bi, Julieth Simon Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Bukombe
MWISHO

0 Comments