Na Shushu Joel, Bukombe.
![]() |
Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko akifafanua jambo kwa wananchi namna gani wanatakiwa kipendana(NA SHUSHU JOEL) |
NAIBU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe. Dkt Dotto Mashaka Biteko ametoa wosia kwa wananchi wa Jimbo la Bukombe na Watanzania kwa ujumla kuendelea kupendana.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la Bukombe na wengine Mbalimbali waliofika kwenye sherehe za kuupokea mwaka 2024 na kuaga mwaka 2023 zilizofanyika nyumbani kwao kata ya Bulangwa.
Naibu waziri Mkuu alisema kuwa watanzania tunapaswa kupendana ili kuendeleza utamaduni wetu ambao tumeachiwa na wazee wetu kwani wao walipendana ndio maana walifanikiwa kutuletea uhuru wa Taifa letu.
" Kuna jirani mmoja alikuwa anafuga paka na mwingine alikuwa anachangamoto ya panya ndani yake ,siku moja ilitokea ajali ya moto kwa mwenye panya bahati mbaya panya mmoja akakimbilia kwa jirani huku akiwa anaungua moto na nyumba ya mwenye paka ikaungua hivyo msemo huu unatufundisha upendo" Alisema Dkt Biteko.
Aidha amewaambia wananchi kuwa tuendelee kutegemea makubwa kwa mwaka huu kwani Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mwaka huu ni vitendo tu hakuna porojo za maneno mane o.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Geita.
Aliongeza kuwa ni vyema sasa wananchi tukaendelea kuwa walinzi wa miundombinu tunayopatiwa na Serikali kwa kuwa walinzi wa miradi hiyo.
Naye Shiratu Masangija amewapongeza viongozi wote kwa ushauri mzito ambao kila mmoja ametoa kwetu
Mwiso
0 Comments