Na Shushu Joel, Bukombe
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Manjale Magambo wametoa tamko kuwa kwa Mwana chama yeyote yule wa ccm atakayechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama hicho jumuiya ya vijana Mkoa huo utamshughulikia.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo akifafanua jambo kwenye baraza la vijna
Rai hiyo
wameitoa kwenye kikao cha Baraza la vijana la Mkoa huo ambacho kilifanyika wilayani Bukombe ambapo
walikubaliana kuwa kwa kipindi kijacho anayetakiwa kuchukua famu ya nafasi ya
kugombea Urais ni yule kipenzi cha Watanzania ambaye ni Dkt Samia Suluhu Hassan
hivyo hakuna mwingine wa kuchukua famu ya nafasi hiyo.
Alisema kuwa
kama Umoja wa Vijana wameamua kutangaza tamko hilo hili jamii ijue kuwa Rais wa
Jamhuli ya Muungano waTanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewakosha watanzania
kwa kuwapatia maendeleo makubwa na ambayo hayajawai kutokea katika nchi hii
lakini kipindi hiki yamefanyika kwa wingi.
“Hivyo sie
kama vijana tunasema ni Dkt Samia Suluhu Hassan ndiye tunakwenda nae 2025 kwani
ameonyesha nia kubwa ya kuwatumukia watanzania” Alisema Manjale
Naye Nelvin
Salabaga ambaye ni mjumbe wa kikao hicho amempongeza Mwenyeki wa Uvccm Mkoa kwa
kufikisha dhamira yetu vijana wa Mkoa wa Geita.
MWISHO
0 Comments