WANANCHI BUKOMBE TUNAMATUMAINI MAKUBWA NA DKT BITEKO.

 Na Shushu Joel 


WANANCHI wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamesema kuwa wanamatumaina makubwa na Mbunge wao ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Mashaka Biteko. 


Wakizungunza mara baada ya kikao wananchi hao walisema kuwa Jimbo la Bukombe limefanikiwa kuwa na wabunge wengi walioliongoza kwa nyakati mbalimbali lakini Mbunge wetu wa sasa Mhe Dkt Biteko amekuwa ni kiongozi wa pekee na mwenue nia nzuri dhidi yetu wananchi wa Bukombe. 


Meshack Joseph ni Mkazi wa wilaya ya Bukombe alisema kuwa wananchi wa Bukombe tuna haki ya kulinga sana kutokana na uwepo wa Mbunge wetu mwenye uchu wa maendeleo kwa wanabukombe. 


Aliongeza kuwa kuwa Jimbo hilo limetawaliwa na wengi lakini Dkt Biteko amekuwa suluhisho la kubwa kwetu wananchi wa Jimbo la Bukombe. 


Aidha amewataka wananchi kuendelea kumuombea Dkt Biteko ili aweze kuwa na afya njema kwa ajili ya kututumikia wananchi wa Bukombe na watanzania kwa ujumla.


Naye Bi, Madha Mahuma (65) mara baada ya kufanya mazungumzo na waandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa Dkt Biteko ni kiongozi shupovu mwenye kutamani kuona maendeleo yakifanyika kwa wananchi wake.


Aliongeza kuwa kuwa Bukombe imekuwa na maendeleo ya haraka kutokana na Mbunge wetu kuwa mpiga kazi za wananchi pasipo kubagua kata.


" Endelea hivyo hivyo kwani sisi wananchi wako wa Bukombe tunakiona kile unachokifanya jimboni" Alisema Bi Madha.


Aidha alisema kuwa Bukombe sasa imefunguka katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kufanya kukua kwa haraka kwa maendeleo na hiki ndicho wananchi wa wilaya ya Bukombe tulikuwa tukihitaji.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments