
Picha ya pamoja ya viongozi wa CCM wilaya ya Bukombe mara baada ya kikao kazi( NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza na kamati tendaji za jumuiya zote za chama katibu wa CCM Wilaya hiyo Ndugu Leonard Mwakalukwa alisema kuwa ni vyema kuongeza idadi kubwa ya uvunaji wanachama wa chama cha mapinduzi.
Alisema kuwa ni vyema kila kiongozi wa tawi na wa kata
kuhakikisha anatemelea wananchi wa eneo lake na kuwaeleza mazuri yanayofanywa
na viongozi wa CCM chini ya Mwenyekiti wa Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan na hasa
yale ya maendeleo kwa watanzania ambao walikuwa na kiu kuwa kuona miradi
mikubwa ikifanyika.
“Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Bukombe imetekeleza
ilani ya uchaguzi kwa asilimia kubwa sana kwa wananchi hivyo tunajivunia kuwa
na viongozi wenye kutekeleza ahadi zao kwa vitendo kwa jamii” Alisema
Mwakalukwa
Aidha katibu huyo wa CCM amempongeza kuwa jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa
Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali
wa mbele katika ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Bi, Julieth Simon amemsifu
katibu kwa kuzidi kuwa mbunufu juu ya uvunaji wa wanachama wapya katika kipindi
hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na ukle uchaguzi mkuu
hapa mwakani.
Aidha amewataka viongozi wa chama na jumuiya kuweza
kuyafanyia kazi maono yanayoelezwa na viongozi wetu ambayo yamekuwa na malengo
ya kujenga chama chetu.
MWISHO
0 Comments