Na Shushu Joel, Bukombe
![]() |
| Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Bukombe Juve akifafanua jambo kwa wajumbe( NA SHUSHU JOEL) |
MJUMBE wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na Mlezi wa kata ya Bulangwa Ndugu Juvenary Mlashan amewaahidi viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bulangwa kuwasaidia katika ujenzi na ukuaji wa Chama katika kata hiyo .
Juve aliahidi hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa kata hiyo ambapo amewataka kuendelea kuwa na umoja ,Upendo na mshikamano ndani na nje ya Chama.
Aidha katika kikao hicho Juve aliahidi kutoa baiskel kwa baadhi ya viongozi wa matawi ambao wamekuwa wakipatwa na changamoto za kuwafikia wanachama na wananchi kwa ujumla kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.
" Tuendelee kuwa na Upendo na Umoja kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili tuweze kushika dola tena hata hivyo viongozi wetu Mbunge Dkt Dotto Biteko na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wanafanya kazi kubwa nasi tuwaheshimishe kwa kuipa ushindi CCM" Alisema Juve
Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Bulangwa Alexanda Mtuzya amempongeza Mlezi wa kata hiyo na mjumbe wa kamati ya Siasa Juve kwa jinsi ambavyo amekuwa nguzo ya kuwaunganisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata ya Bulangwa.
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka viongozi wa CCM kuendelea kutembea kifua mbele kutokana na jinsi viongozi waliowachagua kuweza kuitendea haki kata hiyo ya Bulangwa ikitofautiana na miaka ya nyuma kwani Diwani, Mbunge na Rais wametuwekea alama isiyozibika kata ya Bulangwa.
MWISHO


0 Comments