RAIS DKT SAMIA NI TUNU TUMLINDE" MGALU

Na Shushu Joel, Kibaha 


MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe. Subira Mgalu amewakumbuka watanzania wote popote pale walipo kuendeleza maombo ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani ni Tunu tuliyotunukiwa na Mungu.

Mbunge wa Mkoa wa Pwani Mhe. Subira Mgalu akisisitiza jambo 

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa hadhara katika kata ya Nia Njema Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani


Aliongeza kuwa mpaka sasa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi katika Taifa hili hivyo ni vyema kila Mtanzania kuzidisha maombi ili Munge aendelee kumpatia Rais wetu Afya njema na uendelevu wa kuwatumikia watanzania.


" Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amezidi kuwa kiongozi wa kuigwa sio tu nchini bali hata nje ya mipaka ya Tanzania hii yote ni kutokana na utendaji wake uliotukuka kwa kuwashushia miradi ya maendeleo watanzania kila sehemu" Alisema Mbunge wa Mkoa wa Pwani Mhe Subira Mgalu.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nia Njema  Abdul Pyallah amemsifu Mbunge wa Mkoa wa Pwani kwa jinsi ambavyo amekuwa kioo cha wana Pwani na hasa katika kuelezea  miradi mingi iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Taifa hili.


Aidha amewakumbusha wananchi kuendelea kuitunza miradi hiyo ili iendelee kutoa huduma kwa vizazi na vizazi.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments