RAIS DKT SAMIA NI MWIBA WA MAENDELEO: SUBIRA MGALU.

 Na Shushu Joel, Pwani 


MBUNGE wa Mkoa wa Pwani Mhe. Subira Mgalu amemsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuwa Kiongozi mwenye uchu mkubwa wa maendeleo kwa Watanzania wote



Akizungumza na Waandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA kwenye kipindi maalum cha Book la Dkt Samia kinachoendeshwa na Media hiyo Mgalu alisema kuwa Rais Dkt Samia ameguza nyanja zote za maendeleo ili kuwasaidia watanzania kuweza kupata huduma .


Alisema kuwa katika Nchi hii kumekuwepo na viongozi wengi waliofanikiwa kuongoza Taifa hili na walifanya mambo kipindi hicho lakini kipindi hiki Rais Dkt Samia anazidi  kuweka alama kubwa Watanzania kwani miradi mingi inatekelezeka .


" Miradi ya Umeme,Maji, Miundombinu ya Barabara ,Afya  na mingine mingi nchi nzima imekamilishwa ili kuwasaidia wananchi kuweza kupata huduma" Alisema Mhe Subira Mgalu  Mbunge wa Mkoa wa Pwani. 


Aidha Mgalu aliongeza kuwa ni ngumu kuona maendeleo makubwa yanayofanywa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kama ukiwa utembea Mikoani au Wilayani, tembeenii mtajionea kile kinachofanyika.

Kwa upande wake Diwani wa nia njema amempongeza mgalu kwa kusema yale yanayofanywa na Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hata kuwaelisha wananchi kuweza kutambua kile kinachofanyika

MWISHO

Post a Comment

0 Comments