DR. MKAPA DMO ANAYEKUZA NA KUING'ARISHA SEKTA YA AFYA BUKOMBE.

 Na Shushu Joel, Bukombe 


WANANCHI wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dr. Deograsia Mkapa kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo na hasa wale wanaokwenda kupatiwa huduma za Afya katika hospital ya wilaya na hata kwenye vituo vya Afya vilivyoko kwenye kata mbalimbali

Wakizungumza kwa hisia Wananchi hao walisema kuwa sekta ya Afya ni muhimu sana kwa jamii hasa pale wananchi wanapokuwa wanahitaji huduma hizo pale wanapokuwa na changamoto za kiafya.


Lemi Masanja (62) Mkazi wa kata ya Bulangwa anaeleza kuwa miaka ya nyuma idara ya Afya ilikiwa si ya uhakika kama ilivyo kipindi hiki cha uongozi wa Dr Mkapa ambaye amekuwa akijitoa sana kuhakikisha wilaya ya Bukombe katika sekta ya Afya inakuwa bora zaidi hasa katika utoaji wa huduma kwa jamii.


Aliongeza kuwa Dr. Mkapa amezidi kuwa mbunifu katika sekta ya utoaji huduma kwa wananchi kwani amekuwa akiwaleta madaktari mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya utoaji wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa jamii.


" Hivyo Dr. Mkapa amekuwa msaada sana kwa wananchi wa wilaya ya Bukombe kutokana na ubunifu alionao hivyo huduma zimezidi kuwa imara na bora kwetu wananchi" Alisema Bi, Limi.


Kwa upande wake Dr. Mkapa mara baada ya kuzungumza na HABARI MPYA MEDIA alisema kuwa yote haya yanaonekana katika sekta ya Afya yamefanywa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan huku nguvu kubwa ikitoka kwa Mbunge wetu wa jimbo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu. 


Aidha Dr. Mkapa amewapongeza wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza pindi tunapokuwa na matukio ya upimaji Afya kwa magonjwa ambayo si ya kuambukiza kama vile shinikizo la damu, Kisukari na saratani. 


Hivyo ni vema wananchi wa Bukombe tukaendelea kuiunga mkono serikali yetu ambayo imezidi kuwa imara katika kutuletea vifaa tiba na kutujengea majengo mbalimbali na kuongeza idadi ya wataalamu wa kada mbalimbali 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments