Na Shushu Joel, Bukombe
WANANCHI wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wamempongeza Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko kwa kuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha Bukombe inang'ara kwenye sekta ya maendeleo
![]() |
Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko akifafanua jambo kwa jamii( NA SHUSHU JOEL) |
Maneno hayo yameelezwa na Wananchi wa Bukombe walipokuwa wakizungumza na HABARI MPYA MEDIA kwenye mahojiano maalum.
Salma .. ni mkazi wa kata ya Bulangwa alisema kuwa Mbunge wetu Dkt Biteko amezidi kuwa kiongozi mwenye matamanio ya kuiona Wilaya ya Bukombe inakuwa imara katika katika nyanja ya maendeleo.
Aliongeza kuwa jamii zingekuwa na kiongozi kama Dkt Biteko lazima mjivunie kwani ni mtu mwenye uchu mkubwa wa maendeleo.
Aidha Bi, Salma alisema kuwa wananchi wa Bukombe tuendelee kumuombea kumuombea kiongozi wetu kwa Mungu ili aendelee kutuletea maendeleo wana Bukombe kitu ambacho kilikuwa ni kiu yetu kubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi wilaya hiyo Ndugu Hassan Abdallah alisema kuwa Bukombe tumepata neema kubwa ya kuwa na kiongozi mwenye uchu na maendeleo ya wananchi jambo ambalo limezidi kuwa na neema kubwa kwa wananchi wa Bukombe.
Aidha aliongeza kuwa tangu Dkt Biteko awe Mbunge kumekuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Maji, Umeme,Elimu na Miundombinu.
" Watoto wetu walikuwa wakitumia mwenda mrefu kwenda kutafuta shule lakini jambo hilo sasa ni historia,Wanawake kutembea mwendo mrefu kwenda kujifungua lakini sasa ni historia, Maji na msendeleo mengine yote yanapatikana kwa urahisi jambo ambalo sasa vinapatikana kwa urahisi" Alisema Mwenyekiti wa Wazazi Bukombe.
MWISHO
0 Comments