Na Shushu Joel,Kisarawe
CHANGAMOTO kubwa ya ukataji wa miti kwa ajili ya uchomaji wa mkaa inakwenda kumalizika mara baada ya kumalizika kwa kiwanda cha utengenezaji wa nishati ya makaa ya mawe kukamilika katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
Kiongozi wa mbio za mwenge akipewa maelezo ya kiwanda cha makaa ya mawe na mkurugenzi wa Raslimali watu na utawala wa stamico( NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza katika shughuli za ukaguzi wa kiwanda
hicho ambapo Mwenge wa uhuru umekagua ujenzi huo, Mkurugenzi wa Raslimali watu
na utawala stamico Ndugu Deusdedith Magala alisema kuwa kukamilika kwa kiwanda
hicho ni suluhu la ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mikaa.
“Kukamilika kwa kiwanda hiki kinakwenda kufungua ajira
kwa watu mbalimbali wa wilaya ya kisarawe na wengine wengi” Alisema Mkurugenzi
Raslimali watu na utawala wa STAMICO Magala
Aidha aliongeza kuwa ni vyema sasa watanzania kukipokea kiwanda hicho na kikubwa kununua na kutumia nishati ya makaa ya mawe kwani ni bei nafuu na yenye uwezo mkubwa kuliko matumizi ya mkaa.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenye kitaifa
Godfrey Mzava alisema kuwa ni jam,bo jema serikali ya awamu ya sita chini ya
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya kwa ujenzi wa kiwanda cha makaa yam awe
ambayo yanayokwenda kuwa suluhu ya utunzaji wa mazingira jambo ambalo limekuwa
likipigiwa kelele sana.
Aidha Mzava amewataka stamico kuweza kuongeza nguvu ya
ujenzi wa kiwanda hicho ili kiweze kuanza kazi mara moja.
Pia amewakumbusha stamico kuwa kiwanda hicho
kinakwenda kuhakisi kauli mbiu yam bio za mwenge mwaka huu ambapo inasema
kutunza mazingira na shiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo
mazingira ni yetu lazima tuyatunze kwa nguvu kubwa .
MWISHO
0 Comments