INSPECTOR OSWARD AWAPA SOMO BODABODA.

 Na Shushu Joel, Singida


VIJANA wanaojishughulisha na kazi ya usafirishaji wa abilia kwa njia ya pikipiki maarufu Boda Boda katika kata ya Ikhanoda wilaya ya .. Mkoani Singida wamepewa somo la kujikinga na ajali ambazo si za lazima ambazo zinaweza kuwatokea. 

INSECTOR Osward akifafanua jambo mbele ya wananchi kuhusu mambo mbalimbali


Akitoa elimu hiyo kwa vijana hao wa Boda Boda Inspector wa polisi Mkaguzi Osward Munthary alisema kuwa ni vyema kila mmoja akatambua thamani yake kabla na baada ya kitendo cha kuanza kwa safari ya usafirishaji wa abilia.


Aliongeza kuwa dereva wa Boda Boda unafanya shughuli zako pasipo kuwa na kofia ngumu au pale unapobeba abilia zaidi ya mmoja unakuwa kwenye hatari sana hivyo ni vyema kuzingatia uvaaaji wa kofia ngumu kila unapokuwa katika kazi zako.


"Jambo la usalama katika shughuli za usafirishaji zinatuhusu sote Dereva Boda Boda, Abilia na mtembeaji wa miguu hii ni kutokana na tabia za vyombo vya moto hivyo kila mmoja wetu anapaswa kumlinda mwenzake" Alisema Inspector Osward 


Aidha Inspector Osward amewakumbusha wananchi wa kata hiyo kila mmoja kuzingatia sheria za nchi na kuzitii bila tatizo kwani wanapofanya hivyo wanalisaidia jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake kwa urahisi zaidi.


Naye Mwendesha Boda Boda wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa waendesha pikipiki wamemsifu Inspector Osward kwa jinsi ambavyo amekuwa msingi mkubwa kwa waendesha Boda Boda kutokana jinsi anavyojitoa kuwaelimisha .


Hivyo kwa niaba ya waendesha Boda Boda tutaendelea kuzingatia mafunzo ambayo tunapewa na Inspector Osward 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndugu Jumanne Salimu amempongeza Inspector Osward kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika kata hiyo kwa utoaji wa elimu kwa jamii .


Aidha amemtaka kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwani mafunzo anayoyatoa yanazidi kuwajenga vijana na jamii kwa ujumla.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments