WANAWAKE BUKOMBE WAAPA KUMPA HESHIMA RAIS DKT SAMIA

 Na Shushu Joel, Bukombe 


WANAWAKE wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wameipa kumpa heshima ya pekee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.

Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Akiteta jambo na Naibu Waziri Dkt Dotto Biteko akimpa ufafanuzi wa Jambo ( NA SHUSHU JOEL)


Wakizungumza na HABARI MPYA MEDIA Wanawake hao walisema kuwa sababu za kumpa heshima hiyo ni kama fadhira kwetu kutokana na yale ambayo anatutendea Wanawake wa Bukombe kwani ni makubwa na mengi Rais Dkt Samia anatufanyia.


Salma Hamis ni mmoja wa Wanawake wa Bukombe alisema wao kama Wanawake wa Wilaya hiyo kwa pamoja wamekubaliana kumpa heshima Rais Dkt Samia ili iwe zawadi .


Aidha aliongeza kuwa lengo letu ni kukpatia ushindi wa kutosha katika ngazi za vitongoji na vijiji kwa kuipa kura nyingi CCM. 


Pia alisema kuwa Bukombe ya sasa sio ile ya zamani kwani kazi za maendeleo zinazofanywa na Mbunge wetu wa Jimbo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu amekuwa kiongozi wa pekee katika maendeleo.


Kwa upande Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Bukombe (UWT) Bi Teddy Mageni amewapongeza Wanawake hao kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Aidha katibu huyo amempongeza Mbunge ambaye ni Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko kwa kuwaunganisha makundi yote ndani ya wilaya ya Bukombe.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments