Na Shushu Joel Chalinze.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wameikataa taarifa iliyosomwa na Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira ( DAWASA) kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ubabaishaji wa hali ya juu.
![]() |
Diwani wa kata ya Miono Juma Mpwimbwi akitoa maoni yake kuhusu DAWASA inavyokwamisha wananchi kupata maji ( NA SHUSHU JOEL) |
Akiongoza kikao hicho cha Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Mwinyikondo alisema DAWASA imekuwa ikilalamikiwa na Wananchi mbalimbali wa Chalinze kutokana na huduma mbovu inazozitoa kwa jamii.
Aidha alisema kuwa ni vyema sasa DAWASA wakajipange ili kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora kwa wananchi wa Chalinze kwani kila kukicha ni DAWASA tu jambo ambalo litakuja kutusababishia hasara kubwa kwa wananchi kitu ambacho nasi kama wawakilishi hao hatutaki kuona likitokea.
![]() |
"Tunafuatilia mjadala wa DAWASA kwa makini ila tumekosan imani na meneja kwani maji hayatoki hivyo wananchi wanazidi kuteseka |
Hivyo Madiwani wa halmashauri ya Chalinze kwa ujumla wetu tumekubalina kuwa taarifa hiyo iliwasilishwa na Meneja huyo wa DAWASA hatuko tayari kuipokea kutoka na uongo mtupu uliomo ndani ya taarifa hiyo juu ya utekelezaji wa miradi ya maji Chalinze.
Juma Mpwimbwi ni Diwani wa kata ya Miono alisema kuwa DAWASA wamekuwa wadanganyifu sana kwa wananchi wa Chalinze na mbaya zaidi hata maji yenyewe hayatoki, huduma mbovu wanazozitoa jambo ambalo limetupa maswali mengi kwa wananchi wetu tunaowawakilisha.
Aidha Mpwimbwi aliongeza kuwa DAWASA ni jibu lililoiva na linahitaji kutumbuliwa kwani ni mamlaka ya ajabu sana katika utendaji wa shughuli za usambazaji wa maji kwa wananchi.
![]() |
Diwani akisisitiza jambo juu ya DAWASA inavyowasumbuwa madiwani kujibu maswali mengi ya wananchi kuhusu upatikanaji wa maji |
" Wananchi wamelipia maji kwa kipindi kirefu mbaya zaidi mpaka sasa hawajafutiwa maji kwenye majumba yao na ni zaidi ya miezi 5 sasa kila ukiwauliza vifaa hakuna" Alisema Mpwimbwi.
![]() |
Meneja wa DAWASA akiwasilisha taarifa iliyokataliwa na madiwani wa chalinze |
Kwa upande wake Meneja wa DAWASA Chalinze Eng Felchesm Kimaro amekili kuwepo kwa changamoto hizo ndani ya DAWASA hivyo wataenda kujirekekisha.
MWISHO
0 Comments