Na Shushu Joel, Singida
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida wametakiwa kutambua kuwa kazi ya Polisi ni kazi takatifu ambayo majukumu yake yanahusiana na makatazo na amri za Mungu.
![]() |
Ispector Osward akifafanua jambo mbee ya wananchi waiojitokeza kwenye moja ya mikutano yake anayoifanya kwa jamii. |
Kauli hiyo imetolewa na Inspector wa Polisi kata ya Ikanoda Inspector Osward alipofanya kikao na Wananchi mbalimbali wa kata hiyo
“Makatazo yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu yana mahusiano makubwa na kazi ya Polisi hasa katika amri za Mungu ambazo katika nyumba za ibada wanaziita dhambi huku kwetu ni uhalifu inatupasa kuzuia vitendo hivyo ili jamii iwe salama” Inspector Osward
" Niwakumbushe jambo la muhimu wananchi wenzangu kuwa ni vyema kuwa wamoja katika kutokomeza masuala ya ualifu ili kata yetu iwe takatifu kama yalivyo maandika" Osward
Naye,Mwenyekiti wa kijiji cha Mjughuda kata ya Ikhanoda Athumani Mohamed aliwasisitiza wa i kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia wimbo wa maadili na kauli mbiu ya kazi iendelee hivyo ni vyema kumpa ushirikiano Inspector Osward ili kulifanya kazi ya polis kuwa nyepesi.
MWISHO
0 Comments