BI, MARIAM ULEGA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA.

 Na Shushu Joel, Kibaha.


TAASISI isiyo ya kiserikali ya  Mwanamke Sahihi Fete  yenye Makao yake Makuu Mkoani Pwani chini ya Mwenyekiti Betty Msimbe imemtunuku tuzo ya heshima Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Mkoa wa Pwani Bi, Mariam Ulega.

Bi, Mariam Ulega kushoto akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Mwanamke halisi fete Betty Msimbe( Na SHUSHU JOEL)

Akitoa hiyo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo alisema kuwa taasisi yao imefanya hivyo kutokana na sababu nyingi ilizoziangalia kwa Bi, Mariam Ulega lakini kubwa ni jinsi gani Mama huyo amekuwa kinara wa kujitoa kwenye shughuli mbalimbali za kijamii.


Aidha aliongeza kuwa tuzo hizo zimeshindanisha watu mbalimbali lakini Mariam ulega amepigiwa kura nyingi sana hii inaonyesha jinsi alivyo ni msaada mkubwa kwenye jamii hivyo ni vyema pia jamii kuwaiga watu kama hao.


Aidha Mwenyekiti Msimbe alisema kuwa Bi, Mariam Ulega amekuwa kiungo mzuri kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akijituma kuwatumikia wana jamii wanaomzunguka huku kubwa kujitoa kwa watu wenye mahitaji mbalimbali na kwa hali hii unaweza kutambua ni mtu wa aina gani kwa jamii.


Kwa upande wake Bi, Mariam Ulega mara baada kutunukiwa tuzo hiyo alisema kuwa Tuzo hiyo si yake peke yake bali ni kwa wanawake wote wa Tanzania kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakijituma kusaidia jamii.


Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani yeye amekuwa kiongozi namba moja kwenye kusukuma wanawake kufanya kazi bila kuogopa kitu chochote.


Hivyo Bi, Mariam Ulega amewakumbusha Wanawake wote Nchini kuendelea kuiga kwa vitendo yale mazuri yanayofanywa na Rais wetu kipenzi Dkt Samia. 


Pia niwapongezi Taasisi ya Mwanamke Sahihi Fete kwa kuona mie nafaa kupokea Tuzo hii ya heshima kwangu kwani ni jambo la kujivunia mimi na familia yangu" Alisema Bi Mariam Ulega 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments