WAZAZI BUKOMBE WAELEZEA NEEMA YA MIAKA 3 YA DKT SAMIA.

Na Shushu Joel, Bukombe 


JUMUIYA ya Umoja wa Wazazi wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imeelezea neema kubwa inayozidi kufanya katika wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. 


Akizungumza juu ya kutumiza kwa miaka 3 ya Rais Dkt Samia madarakani Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya hiyo Ndugu Hassan Abdallah alisema kuwa kila Mtanzania anaona kile kinachofanywa na Rais SSH hivyo ni vyema kuendelea kumsemea.


Alisema kuwa kila kiongozi anapokuwa kwenye madaraka anafanya jambo jema kwa wananchi wake lakini Dkt Samia amekuwa mkombozi mkubwa kwa watanzania kwani hakuna sekta ambayo haijaguswa hii inatokana na uhodari wake wa kusaka fedha na kuelekeza kwenye maendeleo sehemu mbalimbali za wananchi.


Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mbali na maendeleo ambayo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anazidi kuyafanya amefanikiwa pia kuimalisha mahusiano na mshikamano ndani ya chama cha Mapinduzi kitu ambacho kilikuwa kiu kubwa ya wana CCM. 


Hivyo jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukombe itaendelea kumsemea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Wananchi ili iweze kutambua yale ambayo Mama anayafanya kwa jamii zetu na nzuri zaidi mpaka sasa hakuna kilichosimama tangu mtangulizi wake atangulie mbele ya haki .


Naye Vero Ibrahimu mkazi wa Uyovu amemsifu Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili kina Mama kwa kiwango kikubwa ambazo ni Afya, Maji na Umeme.


Aidha alisema kuwa hakika Mama amewatendea haki kwa kiwango kikubwa wanawake hata kusaidia kwa asilimia kubwa kuimalika kwa ndoa zao ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo wanawake walikuwa wakitumia muda mwingi kutembea kilometa nyingi kwenda kujifungua na kutafuta maji lakini sasa hivi maji na huduma za Afya ni za Uhakika.


Hivyo alisema kuwa ni vyema wanawake tukawa mstali wa mbele katika kuhakikisha tunalinda miradi hiyo ili iendelee kutumika kwa muda mrefu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments