HAMOUD JUMAA KIONGOZI KINARA PWANI USHIRIKI MASUALA YA KIJAMII.

Na Shushu Joel, Pwani.

WANANCHI wa Mkoa wa Pwani wamempongeza aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kibaha Vijijini Ndg Hamoud Jumaa kwa jinsi ambavyo amekuwa akionekana kwenye matukio mbalimbali ya kijamii ndani na nje ya Mkoa wa Pwani.


Hassan Ally ni mkazi wa Mlandizi amefanya mazungumzo na Mwandishi wa Habari wa HABARI MPYA MEDIA na kusema kuwa Mkoa wa Pwani umebarikiwa kuwa  na viongozi wengi wa kisiasa lakini Alhaji Humoud amekuwa wa pekee sana kutokana na moyo wake wa kujitoa kwa jamii.

Aidha amemtaka kuendelea na moyo huo huo kwani atakuwa na amana yake kwa Mungu hivyo hata Mungu anamuongezea kutokana na kile kidogo anachokipata kuwasaidia wahitaji.


Mwajuma Pili ni Mkazi wa Kibaha amesema kuwa viongozi kama Alhaji Humoud ni wachache katika Taifa letu hivyo ni vyema watu kama hawa wakatazamwa kwa jicho la Tatu.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments